Kuna watu ambao huamini hakuna mapenzi ya kweli duniani, na kuna wanaokubali mapenzi ya kweli yapo. Na hawa wotewanaongea kutoka katika maisha ambayo wameishi, mazingira wakiyokulia, mambo waliyoshuhudia, waliyosoma na pengine waliyofanyiwa. Pamoja na yote hayo bado haiondoi ukweli kwamba mapenzi imekuwa mada na swala linaongelewa sana Ulimwenguni kote. Watu wameua kwa sababu ya mapenzi, watu wameumwa, wamejeruhi, wamejenga uadui kwa sababu ya jambo hili mapenzi.