• Vipande 26 Vya Keki

    0

    Zipo kanuni tu ambazo endapo zitafuatwa zinaweza kumuongoza na zisipofuatwa zinaweza kumuangusha binadamu katika maisha yake ya kila siku na cha ajabu zaidi kwenye hayo maisha, unaweza kufuata kanuni na ukakosa kufaulu na ukaacha kufuata kanuni na bado ukaweza kufaulu.

    Sh25,000.00
    Add to cart
  • Siri ya Kuwaza na Kupanga Kimkakati

    0

    Kitabu kinaeleza uhusiano wa mawazo na mafanikio. Umuhimu wa kuandika mpango badala ya kuwa nao kichwani, uhusiano wa mawazo na matokeo, shauku, uchu na hamu ya kupanga na kutimiza malengo na ndoto pamoja na sababu 5 za umaskini.

    Sh15,000.00
    Add to cart
  • Kustaafu

    0

    Kustaafu ni lazima, hivyo ni vizuri kujiandaa. Kupitia kitabu hiki cha kustaafu kuna aina 12 za mazingira bora yanayoleta tija kabla ya kustaaafu, kazi 5 za kufanya baada ya kustaafu, maeneo ya kujianda kabla ya kustaafu, mikakati 7 ya kuishi maisha marefu baada ya kustaafu, mambo 7 ya kuzingatia kabla hujatumia pensheni n.k

    Sh35,000.00
    Add to cart
  • Kuongeza Thamani

    0

    Kanuni/siri kubwa ya watu au biashara zilizofanikiwa kwa viwango vya juu ni kuongeza thamani. Kama unataka kuongeza utajiri utakaodumu ni kuongeza thamani ya kile unachofanya. Kitabu hiki kitakufundisha namna ya mbinu utakazoweza kutumia katika kuongeza thamani ya bidhaa, huduma, na maisha ya watu kwa ujumla.

    Sh15,000.00
    Add to cart
  • Hisa Akiba na Uwekezaji

    0

    Hisa ni mali fedha. Ndani ya kitabu hiki utapata kujua kwa undani hisa ni nini, faida zake, faida za hisa, changamoto na soko lake. Pia utajifunza mambo ya kuzingatia kabla ya kununua hisa kama vile utaratibu wa kununua na kuuza hisa.

    Sh35,000.00
    Add to cart
  • Hekima Maarifa na Ufahamu

    0

    Hekima, maarifa na ufahamu huondoa umaskini, ujinga, migogoro, hasara n.k. Kitabu kinaeleza tofauti kati ya hekima, maarifa na ufahamu, sifa zake, mikakati ya kupata na kuongeza hekima, maarifa na ufahamu ili ufanikiwe kifedha, kiuchimi, kisisasa kijamii, uongozi na huduma.

    Sh15,000.00
    Add to cart
  • Fursa za Mafanikio

    0

    Mwandishi ametambua namna watu wengi tunatamani kupata fursa lakini zinapokuja hatuchukui hatua kwa kuanza kutafuta ugumu wa fursa hiyo kabla hatujaichukua hatimaye fursa zinatupita. Kitabu hiki kitakufundisha namna ambavyo fursa ndogo zinaweza kukuletea mafanikio makubwa, heshima pamoja na makosa ya kuepuka ili tutwae fursa hizo pamoja na mikakati mbalimbali ya kuzingatia.

    Sh15,000.00
    Add to cart
  • Biashara Bora

    0

    Zaidi ya asilimia 80 ya biashara mpya hufa kabla ya kutimiza miaka miwili. Hapa utajifunza aina za biashara bora, mambo ya kuzingatia kabla ya kuanzisha biashara, sifa na tabia za biashara bora ili uanzishe, uzalishe, umiliki na uwekeze katika biashara.

    Sh15,000.00
    Add to cart
  • Ongeza Kipato Chako

    0

    Kama unatamani kuongeza kipato chako kwa sasa na kuwa na uhakika wa kuendelea kuwa na kipato kinachojitosheleza hadi pale utakapozeeka na uache urithi mzuri kwa kizazi chako kinachofuata, kitabu hiki kitakufaa sana kwa sababu utapata ufahamu sahihi juu ya fedha, uwekezaji na biashara na katika namna unayoweza kufanyia kazi kuanzia leo. Utajifunza jinsi ya kupanga bajeti yako ili upate ziada ya akiba na uwekezaji, pia kutengeneza mkakati wa muda mrefu wa kupata uhuru wa kifedha.

    Sh15,000.00
    Add to cart
  • Timiza Malengo Yako

    1

    Je una malengo ya kufanikiwa katika maisha yako? Kitabu hiki kinatoa mbinu ambazo wengi wamezitumia na wanaendelea kuzitumia duniani kote ili kufikia malengo waliyojiwekea katika maisha yao. Ukweli ni kuwa watu hawashindwi kutimiza malengo yao kwa sababu hawana uwezo na shauku ya kufanya hivyo, bali kwa sababu wameshindwa kujua wafanye nini ili kutimiza malengo waliyonayo katika maisha yao. Katika kitabu hiki utajifunza mambo kadhaa ikiwemo namna ya kuweka malengo yanayofanikiwa. kujua kusudi lililofanya uzaliwe. Mbinu za kuifanya ndoto yako kuwa uhalisia

    Sh20,000.00
    Add to cart
  • Saikolojia ya Mteja

    0

    Katika Biashara yoyote ambayo mtu anaifanya awe anatoa huduma au anauza bidhaa, moja ya uwezo mkubwa sana anatakiwa kuwa nao ni uwezo wa kuhudumia wateja. Na hii imekua ni changamoto kwa watu wengi. Kitabu hiki kimeandaliwa maalumu kwa ajili ya kukupatia maarifa sahihi juu ya saikolojia ya mteja na utajifunza mambo mengi yatakayobadilisha ufahamu wako juu ya mteja.

    Sh15,000.00
    Add to cart
  • Hazina ya Penzi

    0

    Kuna watu ambao huamini hakuna mapenzi ya kweli duniani, na kuna wanaokubali mapenzi ya kweli yapo. Na hawa wotewanaongea kutoka katika maisha ambayo wameishi, mazingira wakiyokulia, mambo waliyoshuhudia, waliyosoma na pengine waliyofanyiwa. Pamoja na yote hayo bado haiondoi ukweli kwamba mapenzi imekuwa mada na swala linaongelewa sana Ulimwenguni kote. Watu wameua kwa sababu ya mapenzi, watu wameumwa, wamejeruhi, wamejenga uadui kwa sababu ya jambo hili mapenzi.

    Sh15,000.00
    Add to cart
  • Malezi Yenye Tija

    0

    Jamii ya sasa ina changamoto nyingi na nyingine hazikwepeki, yapo maendeleo ya kiteknolojia, kiviwanda, kiuchumi na kijamii. Maendeleo haya tukubali au tusikubali yanaathiri eneo la familia na malezi kwa kiasi kikubwa sana. Leo tunashuhudia ongezeko kubwa sana la wazazi wanaolea watoto bila mzazi mwenza. Changamoto hii imenifanya kuandika kitabu hiki ili kumsaidia mzazi, mlezi na yeyote mwenye mawazo ya kuja kuwa na familia huko mbeleni ili kuweza kupata ujuzi na uelewa wa mambo ya ndani kabisa yahusuyo malezi ya watoto wetu. Hakuna aliyezaliwa na ujuzi mkubwa wa malezi. Tunajifunza na tunafundishana. Nikutakie wakati mwema na akili iliyotulia katika kusoma na kukifurahia kitabu hiki. Kusoma tu hakutokusaidia sana. Msaada na manufaa makubwa utayapata pale ambapo utaamua kukiweka kitabu hiki katika matendo.

    Sh15,000.00
    Add to cart