• Ngongoti Shujaa wa Taifa

    0

    Wengi tumekua tukiangalia filamu na kusoma hadithi za Spiderman, Superman, na Batman, ni wakati umefika sasa watoto wa Tanzania na Afrika wawe na mashujaa wao. Mashujaa wanaoweza kusambaza mila na maadili tajiri ya Kiafrika huku kukiwa na wimbi kubwa la utandawazi, ambalo linahatarisha kuharibu utambulisho wetu wa kitamaduni. Hiyo ndiyo kusudi halisi la BETA KIDS, BETA KOMICS, na BETA PANTHA Tunapoitambulisha kwenu tamthilia/kitabu cha NGONGOTI SHUJAA/NGONGOTI THE SUPERHERO, mfululizo wa vitabu vya mashujaa wa kwanza kutoka Tanzania. Pata nakala leo na ulete furaha kwa watoto wako na hata watu wazima pia.

    Ngongongoti yuko hapa kuwaongoza watoto wako katika:

    1. Kujenga kujiamini
    2. Kuelewa aina mbalimbali za unyanyasaji
    3. Kuhimiza ubunifu na uvumbuzi
    4. Kuthamini utamaduni wa Mtanzania
    5. Kuunganishwa na mazingira ya Tanzania
    6. Kukuza ujuzi wa uongozi
    7. Kuheshimu wazazi, wazee, na walimu
    8. Kuthamini kazi
    9. Kupata stadi za maisha
    10. Uhifadhi wa mazingira

    Sh40,000.00
    Add to cart
  • Usichokijua Kuhusu Malezi

    0

    “Mzazi Okoa Hatima ya Mtoto”

    Sh25,000.00
    Add to cart
  • Malezi Yenye Tija

    0

    Jamii ya sasa ina changamoto nyingi na nyingine hazikwepeki, yapo maendeleo ya kiteknolojia, kiviwanda, kiuchumi na kijamii. Maendeleo haya tukubali au tusikubali yanaathiri eneo la familia na malezi kwa kiasi kikubwa sana. Leo tunashuhudia ongezeko kubwa sana la wazazi wanaolea watoto bila mzazi mwenza. Changamoto hii imenifanya kuandika kitabu hiki ili kumsaidia mzazi, mlezi na yeyote mwenye mawazo ya kuja kuwa na familia huko mbeleni ili kuweza kupata ujuzi na uelewa wa mambo ya ndani kabisa yahusuyo malezi ya watoto wetu. Hakuna aliyezaliwa na ujuzi mkubwa wa malezi. Tunajifunza na tunafundishana. Nikutakie wakati mwema na akili iliyotulia katika kusoma na kukifurahia kitabu hiki. Kusoma tu hakutokusaidia sana. Msaada na manufaa makubwa utayapata pale ambapo utaamua kukiweka kitabu hiki katika matendo.

    Sh15,000.00
    Add to cart