Mwandishi ametambua namna watu wengi tunatamani kupata fursa lakini zinapokuja hatuchukui hatua kwa kuanza kutafuta ugumu wa fursa hiyo kabla hatujaichukua hatimaye fursa zinatupita. Kitabu hiki kitakufundisha namna ambavyo fursa ndogo zinaweza kukuletea mafanikio makubwa, heshima pamoja na makosa ya kuepuka ili tutwae fursa hizo pamoja na mikakati mbalimbali ya kuzingatia.