Emilian Busara (MBA, CPA) na Mrembo Grace (MPM, BBA) wana taaluma mbalimbali katika uongozi katika biashara, miradi na fedha. Wameandika zaidi ya vitabu 20 kama vile fursa za mafanikio, maono na malengo, kazi, kipaji, hisa akiba na uwekezaji, n.k. Busara amefanya kazi katika taasisi mbalimbali kama vile Ernst & Young, Plan international, African Wildlife Foundation, EngenderHealth, Management and Development for Health, n.k. Pia ametumikia kama mjumbe wa bodi wa Citi Bank, DSE, World Vision, Vision Fund, TradeMark Africa, Equality for Growth na VSO Jitolee