Bukika inasirikiana na waandishi wa vitabu vya Kitanzania kutatua changamoto ya access ya vitabu nchini.
Tumetambua kwamba mwandishi angeweza kwenda kwenye kituo cha televisheni au kituo cha redio, akafanya makala watu wakapiga simu. Zinaweza zikaja simu nyingi, mia tano, mia sita…
Lakini changamoto hutokea kwenye namna ya kumfikia mtja iliopo vijijini au nje ya makao makuu ya miji.
Imekua ni changamoto sana ambayo ilikua inapelekea kitabu kina weza kika ongezeka gharama mara mbili kwa sababu ya usafiri au ikawa tu haiwezekani kuwafikishia wasomaji pale walipo.
Bukika Books LTD. kupitia mtandao wake ambao umeenea nchi nzima na kupitia logistic partner ambae anafanya kazi nae, Tutume Worldwide LTD, kampuni dada.
Lengo letu kuu ni kuhakikisha kufikisha kitabu pale mteja alipo, ndani ya masaa 24, popote Tanzania!