MUDA ni mali. Sote tunafahamu. Mwenyezi Mungu kwa kulitambua hilo, alimpatia kila mmoja wetu bila kujali hadhi yake katika jamii, kiwango chake cha elimu, uwezo wake wa kifedha, dini yake, kabila lake, jinsia yake, mzunguko wa saa 24 kila siku kuendesha maisha yake. Mzunguko huo ulio sawa kwa kila mmoja wetu ndio mtaji wa kwanza tulionao katika maisha. Uwezo wa kuchagua kipi kifanyike na kipi kingoje ndio hasa unaotufanya tuwe tofauti. Kuna nyakati kwa mfano, tunafanya mambo mengi kwa wakati mmoja kiasi kwamba tunajikuta tunashindwa kuyafanya yale yaliyo muhimu zaidi kwa ufanisi.
Umuhimu wa Vipaumbele katika Maisha
Kitabu cha “Essentialism” kilichoandikwa na Greg McKeown kinajaribu kukupa kanuni zinazoweza kukusaidia kupangilia vipaumbele vyako. Katika kitabu hiki, Greg anawachambua watu wenye hulka ya kufanya vitu vichache kwa ufanisi na wale wanaofanya vitu vingi kwa wakati mmoja. Greg anatumia ulinganisho huo kuja na kanuni unazoweza kuzitumia kufanya vitu chache kwa ufanisi badala ya kujaribu kufanya kila kitu na mwisho wake ukajikuta huna cha maana unachoweza kukionesha kama matokeo yake. Nukuu kubwa ninayoikumbuka kwenye kitabu hiki ninayofikiri inabeba maudhui ya kitabu hiki ni, “Usipojiwekea vipaumbele katika maisha, mtu mwingine atakuchagulia.”
Utafiti wa Martin Seligman na Uchaguzi wa Vipaumbele
Hoja kubwa inayojengwa kwenye kitabu hiki ni kwamba kujaribu kufanya kila kitu hakukutofautishi na mtu asiyefanya chochote. Mtu mvivu anayeamua kukaa bila kufanya chochote hawezi kuwa na kitu anachoweza kuonesha kama matunda ya kazi. Lakini kwa upande mwingine, na mwenzake anayefanya kila kitu bila kuwa na kipaumbele, naye kama huyo wa kwanza, ataishia kushindwa kufanya kitu cha maana katika ufanisi wake. Mwandishi anajenga hoja yake kwa kutumia utafiti uliofanywa awali na Martin Seligman. Seligman alitumia mbwa waliowekewa ‘shoti’ ya umeme. Mbwa wale walitakiwa kuvuta kitufe kilichosaidia kuzima ‘shoti’ ya chumba chao na sio kwa ajili ya chumba walikokua mbwa wengine. Baadae mbwa wale waliwekwa kwenye sanduku kubwa lililokuwa na ukuta unaotenganisha mahali penye ‘shoti ya umeme’ na kule kusikokuwa na ‘shoti’.
Matokeo yalionesha kuwa mbwa waliokuwa wameachwa wawe na uwezo wa kuzima ‘shoti’ walirukia kwenda sehemu isiyo na ‘shoti’ lakini wale waliokuwa kwenye sehemu isiyo na ‘shoti’ hawakuhangaika. Mbwa waliokuwa hawana changamoto, mwandishi anasema, hawakutumia ‘maarifa’ yoyote kwenda kwingine. Hawakutumia nguvu ya maamuzi waliyokuwa nayo kama wenzao waliokuwa kwenye mazingira magumu. Katika maisha, mwandishi anasema, tunapokuwa tunajaribu kufanya kila kitu, tunageuka kuwa kama mbwa wanaoshindwa kuamua wafanye nini. Siku nzima unapojisemesha, “Lazima nifanye hiki, lazima nifanye kile,” unajikuta umewapa watu wengine nguvu ya kukuamulia kipi cha kufanya na kipi usikifanye. Hoja ya mwandishi ni kujifunza namna ya kuhama kutoka kwenye ‘lazima nifanye hiki’ kwenda kwenye ‘nimechagua kufanya hiki.’
Kanuni ya 90: Kuwa Mhariri wa Maisha Yako
Hapa tunajifunza somo la pili muhimu katika maisha. Ukitaka kuwa mtu unayejiwekea vipaumbele, lazima kwanza ujifunze kuwa mhariri wa maisha yako. Kanuni moja wapo ya kufanya hivyo ni ile ambayo Greg anaiita ‘kanuni ya 90,’ ambayo kimsingi inakutaka kupima uzito wa kila unachotaka kukifanya. Iwe ni maamuzi, kazi ya kufanya au majukumu uliyoyaorodhesha, lazima uyape alama kati ya 0 mpaka 100. Jukumu lolote unalolipa alama chini ya 90 achana nalo. Lakini ili kujua uzito wa jukumu lako, anza na kujiuliza namna shughuli hiyo au maamuzi hayo unayotaka kuyafanya yanavyokuwezesha kufikia malengo yako mapana. Jiulize, “Hiki ninachotaka kukifanya, kinanisaidiaje katika safari yangu ya kufikia ndoto nilizonazo?” Ukiwa mtu mwenye dira ya maisha inayoeleweka, mtu unayejua kitu gani unataka kukifanya, majibu ya swali kama hilo yatakusaidia kusema ‘hapana’ kwa shughuli nyingi ambazo kimsingi ni upotevu wa muda usio na sababu.
Mfano wa Walgreens: Kuchukua Hatua za Kistratejia na Teknolojia
Somo la tatu kubwa, ni kujifunza kuongeza asimilia 50 ya muda uliojipangia kufanya kile ulichoamua kukifanya. Hiyo ndio raha ya kusema hapana kwa vitu visivyokusaidia kufikia malengo yako. Unapokuwa na vitu vichache vya kufanya hiyo haimaanishi utajikuta saa nyingine huna kitu cha kufanya. Hapana. Uchache wa majukumu unakupa muda wa kutosha kuweka akili yako kwenye kile ulichoamua kukifanya. Kwa mfano, ukiamua kuwa na vitu vitatu tu vya kufanya kwa siku, kuna uwezekano wa kujikuta unatumia muda mwingi zaidi kuliko vile ulivyokuwa umepanga. Sababu ni kwamba mara nyingi tuna hulka ya kukadiria muda kidogo kwa shughuli kubwa. Ndio maana mwandishi anashauri kwamba unapopangilia majukumu yako, jiongezee asilimia 50 ya muda zaidi kukuwezesha kukabiliana na yale yasiyotarajiwa. Unapofikiri kuandika makala kutachukua saa moja kuikamilisha, ongeza dakika 30 kwenye ratiba yako. Unapofikiri utatumia saa 6 kukamilisha ripoti, ongeza saa 3. Utaratibu kama huu utakusaidia kupumua na hivyo kutokufanya vitu kwa kukimbizana na makataa (deadline). Tunachokifunza hap ani kwamba kujiongezea muda ni mbinu muhimu sana ya kuhakikisha muda wako unatumika zaidi kwenye majukumu ya muhimu zaidi yanayokuwezesha kufikia malengo yako.
Kujiongezea Muda kwa Majukumu Muhimu
Somo la tatu, na kubwa, ni kwamba katika biashara ni muhimu kukabiliana na ukweli kwa wakati. Makampuni yanayofanya vizuri, kwa mujibu wa Jim Collins, yana tabia ya kuukubali ukweli mchungu mapema na kuchukua hatua za kuufanyia ukweli mapema. Makampuni haya hayafanyi kama afanyavyo mbuni anayejifariji kwa kuficha kichwa chake mchangani wakati mwili wote uko nje. Lakini pia, hunyanyui mikono juu ishara kuwa umekata tamaa.
Unapoona dalili mbaya katika biashara, labda mauzo yamepungua kwa mfano, chukua hatua haraka. Usitumie uzoefu wako wa zamani kujifariji kuwa mambo yanaweza kubadilika. Unapoona sera za serikali zinabadilika tofauti na ilivyozoeleka, una kazi ya kujichunguza na kuona namna gani mabadiliko hayo yanaweza kuathiri utendaji wa shughuli zenu na hivyo kuchukua hatua kwa wakati. Usipofanya hivyo unajiweka kwenye hatari ya kujikuta unafunga biashara. Kwa upande mwingine, kuchukua hatua kunategemea kiwango cha ujasiri ulichonacho. Mambo yanabobadilika, usikimbilie kulalamika na kusubiri kupotea kwenye biashara. Lazima kuchukua hatua kwa ujasiri ukijua kuwa kufa kwa kampuni yako kunaweza kuwaathiri wengine lakini mhusika mkuu ni wewe.