Umewahi kujiuliza kwanini tunashindwa kuishi kwa upendo na heshima na watu wanaotuzunguka kila siku?
Episode hii, Masoud Kipanya anatufundisha juu ya jinsi tunavyoweza kuwadharau au kuwatenga wengine bila hata kujua, tukisahau umuhimu wao kwenye maisha yetu. Pia, anazama kwenye swali zito—jamii ina mchango gani katika malezi ya mtoto, na kwa nini matokeo yake yanaonekana baadaye maishani? Je, ni nani anayebeba lawama pale mambo yanapoenda mrama?
Sikiliza maoni ya Masoud kuhusu masuala haya muhimu kwenye video hii.