Katika Episode hii ya Bukika Stories na Masoud, Masoud Kipanya anafafanua maana ya kupenda na tofauti kati ya kuwa na upendo kwa maneno na kwa vitendo. Anazungumzia msingi wa kujipenda na kuwapenda wengine, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya wema kwa watu. Kupitia kitabu chake Vipande 26 vya Keki, mwandishi anatufundisha kuwa upendo wa kweli unaonekana kwa matendo, si kwa maneno tu.