Kuna wakati unashangaa mtu anafanya jambo ambalo kwa kiwango cha mahusiano yenu uliamini alipaswa kukushirikisha.
Wakati mwingine mtu anafanya uamuzi na ulitamani angekuhusisha…
…hata kama usingebadilisha kitu ila ungeoona amekuheshimu.
Yakitokea mambo kama haya, USIWAKASIRIKIE.
Huwa kuna sababu mbili kubwa:
Moja, kuna mzigo Mungu anakuepusha nao.
Wangekushirikisha kuna gharama ingebidi uingie kwa ajili yao.
Wakati mwingine kwa sababu ya kushirikishwa, ingebidi utumie PESA, MUDA au NGUVU zako ili kuwabeba.
Kwa sababu hawajakushirikisha, wamekupunguzia yote hayo, shukuru.
Mbili, kuna namna Mungu anataka awafundishe kuwa bado wanakuhitaji.
Kitakachotokea ni kuwa wataenda mbele kidogo kisha WATAFELI na watagundua WANAKUHITAJI.
Ungeendelea kuwaambia wewe wasingeelewa, ila kwa yale watakayokutana nayo, watagundua kuwa BADO WANAKUHITAJI.
Usiwakasirikie ukiona hawakushirikishi leo, relax, wape muda, WATARUDI wenyewe.
Jifunze kutogombana na watu kwa sababu haujashirikishwa, wakati mwingine ni kwa faida yako.
Naomba unisaidie kushare na wengine Tafadhali.