Usisahau KUJIPENDA MWENYEWE

Ndio, namaanisha kujipenda na kujifurahisha wewe mwenyewe.

Katika Ulimwengu tuliopo, kila mtu yuko kwenye pilika za kufukuzana na jambo fulani.

Kuna wakati wale ambao ulitarajia wakuoneshe upendo aidha HAWANA MUDA HUO…

…au wanakuonesha kwa namna ambayo ni TOFAUTI na ile ambayo wewe unaitaka.

Badala ya kuendelea KUWALAUMU kwa kile ambacho hawafanyi, JIFANYIE KITU mwenyewe.

Kuliko kuendelea KUSUBIRIA hadi watakapopata muda na NAFASI ya kukufanyia UNACHOTAKA, anza kujifanyia mwenyewe.

Tafuta muda wa kujifanyia vitu vinavyokufurahisha. Pata muda wa KUJITOA OUT mwenyewe.

Pata muda wa KUPUMZIKA kabla haujaishiwa nguvu kabisa.

Pata muda wa kujinunulia NGUO NZURI unazozipenda, saa ya nzuri n.k

USISAHAU kuwa kuna watu wataanza KUJUA unachotaka…

…baada ya kuanza kujipenda mwenyewe na KUONESHA kwa VITENDO.

UNAPOWAFURAHISHA wengine, uwe makini usisahau KUJIPENDA MWENYEWE.

Je, wewe utafanya nini kuanza KUJIPENDA mwenyewe?

Naomba nisaidie kushare makala hii na wengine kama mimi nilivyoshare na wewe.

Ahsante kwa kuwa umeshare.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *